Msanii wa Ufaransa, Abraham Poincheval amefanya tukio hatarishi la kuiishi ndani ya chumba maalum kwa lengo la kutotoa vifaranga wa kuku akitumia joto la mwili wake.
Atakaa kwa muda wa wiki tatu (siku 21 mpaka 26) katika chumba maalum cha vioo akiatamia mayai kumi ya kuku kwa kutumia joto la mwili wake. Watalii wengi wamekuwa wakimuangalia msanii huyo ambaye mpaka sasa ameshatumia muda wa wiki tatu akiwa ndani ya chumba hicho katika makumbusho ya Palais de Tokyo nchini Paris.
“Ukweli ni kuwa nitakuwa kuku” alisema.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 44 alianza tukio hilo alilolipa jina la “Oeuf” lenye maana ya “Mayai” siku ya jumatano ya Machi 15, 2017. Aliyakalia mayai hayo katika kiti kilichowekewa mfuko chini yake.
Poincheval amejifunga blanketi ili kuzuia joto kupotea na anatumia vyakula vinavyoongeza sana joto mwilini kama vile tangawizi.
Wakati wa haja, msanii huyo hatopaswa kuinuka kwenda kujisaidia, badala yake atatumia boksi maalumu lililotengenezwa chini ya kiti hicho.
Ili mayai yaweze kuanguliwa vizuri, anapaswa kuinuka katika kiti hicho kwa muda usiozidi dakika 30 ndani ya saa 24.
Kabla ya kufanya tukio hilo la kuatamia mayai ya kuku, Poincheval amewahi pia kuishi ndani ya jiwe la chokaa lililotengenezwa kwa umbo la yai.
Amewahi pia kuishi ndani ya sanamu ya dubu, katika mfereji ulioko chini ya maktaba na kusafiri ndani ya maji akiwa katika chupa kubwa ya plastiki iliyowekwa mfuniko.
Post a Comment
Post a Comment