const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Spika Tulia awaondoa hofu wakulima wadogo "Ninyi mna haki sawa kwenye rasilimali zetu" - HABARI MPYA

..

Spika Tulia awaondoa hofu wakulima wadogo "Ninyi mna haki sawa kwenye rasilimali zetu"



News

Spika wa Bunge la Tanzania Dkt .Tulia Ackson ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) amesema serikali ipo tayari kuwasikiliza wakulima wakati wowote kwa kuwa wana haki sawa kwenye rasilimali za taifa na kuwaomba wakulima wadogo kuendelea kuweka wazi changamoto zao zinapotokea.

Dkt.Tulia amebainisha hayo mkoani Njombe wakati akifungua mkutano mkuu wa 28 wa maadhimisho ya miaka 30 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) unaofanyika mkoani humo.

"Mna haki sawa kwenye rasilimali zetu kama taifa na ikiwa kuna mahali ambapo mnaona pengine viongozi tumelegea Chama chenu tunakiheshimu sana na tutakuwa tayari kuwasikiliza ikiwa kuna jambo lolote tunalopaswa kulifanya vizuri zaidi"amesema Dkt.Tulia

Steven Luvuga ni mkurugenzi wa MVIWATA Tanzania amesema wakulima nchini wanachangamoto mbalimbali ambapo anaamini serikali inaendelea kutatua changamoto hizo hatua kwa hatua.

"Bado wakulima wanachangamoto mbalimbali ambazo tunaamini hatua kwa hatua zinatatuliwa na kwa kuangalia historia ya taifa letu na hali halisi ya jamii yetu ilivyo tunaamini wakulima wadogo watabaki kuwa moyo wa uzalishaji kwa muda mrefu"amesema Luvuga

Awali mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ametoa pongezi kwa MVIWATA ambao ndio sauti ya wakulima kwa kufanyia mkutano wao mkubwa uliokutanisha zaidi ya wakulima 1000 kwa kuwa umesababisha watu wa Njombe kuchangamana na kujifunza kwa wengine kwa kuwa pia mkoa huo ni miongoni mwa mikoa iliyoshikilia uchumi huku pia wananchi wake wakiwa ni wakulima kwa asilimia kubwa.


Related Posts

Post a Comment