Mwili wa Mwandishi Khashoggi Ulitoswa Kwenye Tindikali Baada ya Kuuawa

Kiongozi wa ngazi ya juu nchini Uturuki, Yasin Aktay, amesema anaamini kuwa mwili wa mwandishi Jamal Khashogi uliyeyushwa kwenye tindikali baada ya kuuawa na kukatwa katwa.

Bw Atkay ambaye ni mshauri wa Rais wa Uturuki Racip Erdogan amesema hitimisho pekee linaloingia akilini ni kuwa waliomuua mwandishi huyo wameteketeza mwili wake "ili kufuta kabisa ushahidi."

Khashoggi, ambaye alikuwa mkosoaji mkuu wa utawala wa Saudia hususani sera za mrithi wa kiti cha ufalme mwanamfalme Mohammed bin Salman aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul mnamo Oktoba 2.

Mwanamfalme wa Saudia aliamini 'Khashoggi alikuwa hatari'
Hiki ndicho kikosi 'kilichomuua' Khashoggi
Zitto Kabwe aachiwa kwa dhamana
Alikimbilia Marekani mwaka 2017 akihofia usalama wake na huko alikuwa akiandika makala na maoni kwenye gazeti la Washington Post.

"Sababu ya kumkata vipande vipande ilikuwa ni kurahisisha kuyeyusha mwili huo kwa wepesi", Bw Aktay ameliambia gazeti la kila siku la Hurriyet.

"Sasa tunafahamu kuwa si tu walikata kata mwili wake vipande bali waliuyeyusha kabisa."
Licha ya kauli hiyo kutoka kwa kiongozi mkubwa, bado hakuna ushahidi wowote wa kiuchunguzi uliotolewa unaothibitisha kuwa mwili huo ulitoswa kwenye tindikali. Lakini mpaka hii leo, mwezi mmoja toka auawe, mwili wake bado haujapatikana.

Kauli hiyo imekuja wakati ambao mchumba wa Khashoggi, Hatice Cengiz, akiwataka viongozi wa dunia "kuwachukulia hatua walioshiriki mauaji", katika tahariri iliyochapishwa katika magazeti matano makubwa ya kimataifa, ikiwemo in an editorial for five newspapers, Guardian na Washington Post.

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image caption
Mwanamfalme Mohammed Bin Salman ameiambia Marekani kuwa Khashoggi alikuwa mtu hatari.
Pia hii leo taarifa mpya zimeibuka kuwa mwanamfalme Mohammed bin Salman aliwaambia maafisa wa Marekani kwamba anamchukulia mwanahabari Khashoggi kama mshirika hatari wa kundi la kiislamu lenye itikadi kali.

Mwanamfalme Mohammed ameripotiwa kusema hayo katika mazungumzo yake ya simu na maafisa wa Ikulu ya Marekani baada ya kupotea kwa Khashoggi.
Saudia hata hivyo imekanusha ripoti hiyo iliyochapishwa katika magazeti ya Washington Post na New York Times.

Waendesha mashtaka wa Istanbul wamethibitisha siku ya Jumatano kuwa mwandishi huyo alinyongwa, huku wenzao wa Saudia wakikiri kuwa mauaji hayo yalipangwa.

Haki miliki ya pichaEPA
Image caption
Salah,mtoto wa kiume wa Jamal Khashoggi alipokutana Mwanamfalme Mohammed Bin Salman
Huku hayo yakijiri mtoto wa kiume wa Jamal Khashoggi, Salah pamoja na familia yake wamewasili Marekani siku chache baada ya kukutana na Mwanamfalme Mohammed Bin Salman.


Katika taarifa iliyochapisha magazetini familia nya Khashoggi imekanusha madai kwamba Khashoggi alikua mwanachama wa kundi la Muslim Brotherhood.

Familia hiyo pia imeongeza kwamba yeye mwenyewe aliipinga madai hayo mara kadhaa katika miaka ya hivi karibuni."Jamal Khashoggi hakua mtu hatari kwa vyovyote. Madai hayo ni ya kushangaza sana," ilisema taarifa hiyo.

Mpaka sasa hakuna makubaliono yaliyofikiwa kuhusu jinsi Khashoggi alivyofariki.
Aliingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul kushughulikia stakabadhi za kumwezesha kumuoa mchumba wake wa Uturuki, Hatice Cengiz.

Siku ya Jumatano Uturuki ilisema kuwa aliuawa alipoingia ndani ya ofisi za ubalozi huo na mwili wake kukatwa katika vipande "kulingana na utaratibu uliopangwa awali''.

Vyombo vya habari vya Uturuki viliwahi kuripoti kuwa Khashoggi aliteswa kabla ya kuuawa.
Saudi Arabia imebadilisha kauli yake ya awali kuhusu mkasa wa kutoweka na kuuawa kwa Khashoggi.

Habari za kutoweka kwake zilipoangaziwa kwa mara ya kwanza Saudi Arabia ilisema kuwa Khashoggi alitoka ndani ya ubalozi wake mjini Istanbul akiwa hai.

Related Posts

Post a Comment