Baada ya kukaa nje ya game la bongo fleva kwa muda, Rapa Chidi Benz amefunguka na kusema ameamua kujikita kwenye killimo akishirikiana na mama yake mzazi ili kuweza kujikimu kimaisha.
Leo akiwa kwenye dakika 10 za maangamizi kipindi cha Planet Bongo ndani ya East Afrca Radio Chidi amesema kwamba mama yake ni mtu wake wa kwanza kwenye kumpatia sapoti ndiyo maana anashirikiana naye katika kuwajibika kiuchumi.
"Kwa sasa najishughulisha na kilimo kwa sana. Mimi na mama yangu tuna mashamba huko Chanika kwa hiyo hichi kipindi nilichokaa nje ya 'game' kilimo kinaendeleza maisha yetu japokuwa mimi mkulima wa mjini', alisema Chidi.
Aidha Chidi ameongeza kwamba :
"Lakini nina familia niliyoitengeneza kipindi nafanya vizuri kwenye game kwa hiyo siwezi nikafa na njaa wakati mimi nilikuwa nawalea na kuwasaidia pale walipokuwa wakinihitaji. Wasanii wengi wapo upande wangu hawakumbuki mabaya yangu wengi wanarudisha mawazo yao nyuma kwa mazuri yangu",Chidi Benz aliongeza.
Hata hivyo rapa huyo kwa sasa amerudi na ngoma aliyomshirikisha Mkongwe Q- Chillah inayokwenda kwa jina la 'muda'.
Post a Comment
Post a Comment