Baada ya wiki ya mchakato wa usahili, Mshindi wa Big Brother Africa-Hotshots wa 2014, Idris Sultan ataonekana katika filamu ya ‘Ballin …On the Other Side of the World,’ itayoandaliwa nchini Marekani chini ya muongozaji Harvey White.
Muongozaji wa filamu hiyo aliwahi kufanya kazi na wasanii wenye majina makubwa akiwemo Chris Brown, Mariah Carey, Lady Gaga na Tamia.
Akiwa kama mhariri wa filamu, amehariri baadhi ya filamu kama vile ‘Think Like A Man 2,’ ‘The Wedding Ringer,’ na ‘King of the Dance Hall’ akishirikiana na Whoopi Goldberg.
Hadithi ya filamu hiyo imetungwa na Torino Von Jones, ambapo hadithi hiyo inamhusu kijana mdogo wa Kenya (Kunjani), ambaye wazazi wake ni waathirika wa uhalifu uliojaa vurugu.
Siku moja katika maeneo ya ya shule, kijana huyo aliye na umri wa miaka kumi na tatu aligunduliwa na padri wa Kimarekani ambaye alimwona akicheza mpira wa kikapu na akaamini ana uwezo mkubwa na anaweza kushirikia ligi ya NBA.
Wote wawili waliendelea na urafiki wao na padri huyo alianza kumpatia ushauri. (King) itaigizwa na Sultan, ana haiba kubwa,lakini ni mhalifu mkubwa na hatari sana ambaye ana wazo jingine na anataka Kunjani kujiunga na kundi lake la wahalifu na atafanya kila liwezekanalo ili mpango huo ufanikiwe.
Mara ya mwisho Sultan alionekana katika filamu ya Tanzania ‘Kiumeni,’ ambayo itaoneshwa katika tamasha lijalo la wiki ya filamu la Zanzibar (ZIFF) ambapo ‘Kiumeni’ itaoneshwa wakati wa Siku ya tamasha ya filamu za Kiswahili ya ZIFF Julai 14, na mtayarishaji na nyota wa filamu Ernest Napoleon.
Mapema mwaka huu, Napoleon aliweka historia wakati alipochaguliwa kuwa rais wa kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa filamu ya Marekani ya D Street Media Group yenye makao yake jijini New York, pamoja na ofisi katika miji ya Berlin, Buenos Aires na Cape Town.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa D Street na mtayarishaji mtendaji Dexter Davis walimtambua Idris kutokana na kuiangalia filamu ya “Kiumeni’.
“Idris Sultan has what it takes to become an international star and our upcoming film ‘Ballin… On the Other Side of the World’ is a perfect fit. We’re considering Mr. Sultan for other movies as well, alisema Davis.
Kampuni hiyo ya filamu inaazimia kupiga picha sehemu za Marekani na Kenya na haitachelea kutafuta vipaji vingine kwa waigizaji wa Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania pale inapolazimu.
Filamu hiyo imeandaliwa kwa bajeti ya Dola za Marekani milioni tano.
Post a Comment
Post a Comment