const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Bifu kubwa laibuka kati ya Dani Alves na familia ya Maradona,sababu ni hii - HABARI MPYA

..

Bifu kubwa laibuka kati ya Dani Alves na familia ya Maradona,sababu ni hii

Wiki iliyopita mlinzi wa kulia wa Brazil na klabu ya Juventus Dani Alves alikuwa akifanyiwa mahojiano na kitua kimoja cha habari nchini Brazil, mahojiano ambayo yalidumu kwa muda wa lisaa lizima.

Wakati wa mahojiano hayo mwandishi wa habari alimuuliza swali Alves ambalo limemuingiza matatani sana na familia ya nguli wa zamani wa soka nchini Argentina Diego Maradona.

Muandishi alimuuliza Alves kuhusu ubora kati ya Lioneil Messi na Diego Maradona ambapo Alves bila kupepesa macho alimtaja Lioneil Messi na sio tu kumtaja bali akatoa sababu ya kutomkubali Maradona.

“Unaniuliza nani bora kati ya hao wawili?kwani Maradona amebeba tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara ngapi?Messi ni bora na huwezi jisifu wewe ni bora wakati ulichukua kombe la dunia kwa goli la mkono” alisema Alves.

Dani Alves alienda mbali zaidi kwa kumshambulia Maradona baada ya kusema hawezi kuhadithia hata watoto wake jinsi alivyofunga goli la mkono na huo sio mfano mzuri kwa wachezaji vijana.

Baada ya Alves kusema hivyo, mtoto wa kike wa Maradona aitwaye Dalma Maradona hakutaka kuacha babake ashambuliwe vyote hivyo ikambidi achukue simu yake na kujibu mashambulizi ya Alves.

“Hembu kaa chini na kawaulize Wabrazil wenzako watakuambia baba yangu ni nani kwa jinsi alivyowanyanyasa na nina uhakika wao watakuambia vizuri Maradona ni nani” alisema Dalma.

Dalma alisema kwanza swali la kumfananisha Maradona na Messi ni la kipuuzi na kusisitiza baba yake alikuwa maarufu kipindi ambacho wanasoka wemgi waliokuwa maarufu walikuwa wakitokea bara la Ulaya.

Dalma alizidi kumshambulia Alves kwa kumuambia kwamba baba yake hakucheza soka ili kuwa Role Model wa mtu na kuhusu goli la mkono kama hajalipenda baaasi aangalie magoli mengine.

 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!


Related Posts

Post a Comment