Msimu wa nne wa mashindano ya Ndondo Cup umezinduliwa rasmi Jumamosi Juni 17, 2017 kwenye uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam huku mchezo wa ufunguzi ukizikutanisha Stim Tosha dhidi ya Makuburi na dakika 90 zikamalizika bila timu hizo kufungana.
Mgeni rasmi aliyezindua mashindano hayo alikuwa ni DAS wa Wilaya ya Ubungo James Mkumbo ambae alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.
Msimu mpya wa Ndondo Cup 2017 ndio umeanza, endelea kufuatilia mashindano haya kwa kuhudhuria viwanjani kushuhudia games mbalimbali, unaweza pia kuangalia live kupitia Azam TV na Clouds TV lakini pia kupitia mitandao kama www.shaffihdauda.co.tz, Dauda TV, www.ndondocup.co.tz, pia unaweza kupata habari kupitia mitandao ya kijamii facebook (NdondoCup), Twitter (@NdondoCup) na Instagram (ndondo_cup).
Hapa unaweza kuangalia picha za matukio mbalimbali ya uzinduzi wa Nodndo
Post a Comment
Post a Comment