Miezi iliyopita tuliandika juu ya tetesi za kuwepo kwa mwanamke mmoja ambaye hajulikani ni nani lakini alikuwa na mimba ya mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo, jambo hilo limekuwa siri kubwa katika familia ya Ronaldo lakini hadi mama yake mzazi analijua hilo.
Sasa taarifa mpya zinasema siku ya Alhamisi mwanamke huyo amejifungua watoto mapacha wa kike na wa kiume ambao wanafahamika kwa majina ya Mateo na Eva, kituo kimoja cha habari nchini Ureno kimedai siku sio nyingi Cristiano Ronaldo ataiambia dunia kuhusu ujio wa watoto hao.
Kituo cha televisheni cha SIC kimedai hadi sasa hakuna picha hata moja ambayo watoto hao wamepigwa na kikishindwa kufahamu watoto hao wamefichwa wapi kwa wakati huu lakini kikisema wana uhakika na taarifa hiyo ya kuhusu mapacha wa Cristiano Ronaldo.
Hakuna taarifa yoyote kutoka kwa upande wa Ronaldo wala wakala wake kuhusu hilo lakini blogspot kubwa,website na magazeti makubwa ikiwemo gazeti kubwa kabisa nchini Ureno cha Daily Correio Da Manha limeandika kuhusiana na watoto hao.
Ronaldo ambaye kwa sasa ana mpenzi mpya Georgina Rodriguez inasemekana mwanamke ambaye amezaaa naye ni mwenyeji wa bara la America na hii haitakuwa mara ya kwanza kwa mwanasoka huyu kuzaa na mwanamke asiyejulikana kwani hata mtoto aliyenaye mama yake hajulikani.
Post a Comment
Post a Comment