Wazee wa Simba wametishia kumlaani mwanachama na mdau mkubwa wa Simba Mohammed Dewji Mo kama asipoomba radhi baada ya kauli yake ya kuifananisha klabu ya Simba na mke wake.
Akizungumza kwa niaba ya wazee wa Simba Mzee Felix Mapua amesema, Mo ameidhalilisha Simba na anatakiwa kuomba radhi vinginevyo watamlaani.
“Namtahadharisha huyu bwana mdogo Mohammed Dewji ‘Mo’ tumekapokea mwaka 1999 kupitia kwa mpwa wake Kassim Dewji, achunge mdomo wake hawezi akaifananisha klabu ya Simba na mke wake, ametudhalilisha na kama amelelewa vizuri na kukuzwa wazazi wake basi aombe radhi kama hatoomba radhi tunampa laana.”
“Yeye hajajitolea chochote kuna watu wametoa pesa kuna mzee kununua gari tukawa klabu ya kwanza kuwa na gari leo hii aje aseme anaidai Simba kwa lipi mbona anahamaki baada ya mdhamini kuingia si akae pembeni?”
“Imemshinda African Lyon na Singida United sasa anaifatafata Simba ya kazi gani? Kwa hiyo tunamuomba achunge mdomo wake anapoongea na vyombo vya habari sisi sio watoto wadogo sisi ni baba zake.”
“Simba imemsaidia, kapata ubunge Singida kwa wanachama wa Simba kumfanyia kampeni, yeye kapata umaarufu kwa jina la Simba. Hivi vijisenti vyake visitusumbue yeye ketu ni ka-sisimizi tu.”
Hayo yote yamekuja siku chache baada ya uongozi wa Simba kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa bila kumshirikisha kama walivyokuwa wamekubalia na tayari aliwa analipa mishahara ya wacheza wa klabu hiyo.
Post a Comment
Post a Comment