Golikipa mzoefu wa ligi kuu Tanzania bara anaecheza Mwadui FC amekiri mwenyewe kwa mdomo wake wala simlishi maneno, nyanda huyo amesema, mechi ya Ndondo ni ngumu kuliko ya ligi kuu.
Kado alikuwa anazungumza na Clouds TV mara baada ya kusaini kukipiga na chama lake la mtaani Makuburi SC ya Tabata ndipo akasema Ndondo na ligi kuu unaweza ukalinganisha.
Kado pia akasema Ndondo inaongeza uzoefu kabla ya kucheza ligi kuu kwa hiyo huwa anawashauri vijana wacheze Ndondo lakini pia akasema mechi za Ndondo ni ngumu kuliko za ligi kuu.
“Kabla ya kucheza ligi kuu unapocheza Ndondo kuna ujasiri na uzoefu fulani unaupata, naweza kusema kwenye Ndondo kuna ugumu kuliko ligi kuu,”
“Nawapongeza sana Clouds waandaji wa Ndondo kwa sababu kwa sasa Ndondo na ligi kuu unaweza ukalinganisha.”
Kumbuka kuwa Kado amewahi kushinda tuzo ya golikipa bora wa VPL pamoja na kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Post a Comment
Post a Comment