const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Wimbo wa Acha Nikae Kimya wa Diamond Wakosolewa...Wadaiwa Kuegemea Upande Mmoja - HABARI MPYA

..

Wimbo wa Acha Nikae Kimya wa Diamond Wakosolewa...Wadaiwa Kuegemea Upande Mmoja

Ni katika wimbo wake mpya uitwao bora nikae kimya. Diamond amegusia ugomvi wa Makonda na Gwajima na ushiriki wa Mange. Amegusia tatizo la vyeti la Makonda na shinikizo la kutaka atenguliwe.
Katika wimbo huo mpya amegusia wimbo wa Ney na kukamatwa kwa Ney, kupotea kwa Roma.

Ametumia fasihi ya hali ya juu lakini wimbo huu unamuweka kwenye kundi la waoga wanaohofia maisha yao. Diamond anasema kwenye wimbo huo ameonywa na mama yake juu ya kusema chochote kwa yanayotokea.

Anasema kumekuwa na shinikizo kutoka kwa mashabiki wakimtaka aseme chochote kuhusiana na yanayoendelea na wengine wakimtuhumu kuwa anaogopa kusema kwa kuwa Makonda ni mlezi wa Wasafi.

Diamond anasema alishindwa kupost wimbo wa nay japo ni rafiki yake wa karibu (kwa sababu ya maudhui) lakini aliumia sana Nay alipokamatwa.

Amegusia pia mgogoro ya CCM na CHADEMA.

Ametumia ufundi wa kisanaa hasa kuwasilisha ujumbe wake, lakini wimbo huu unaweza kutafsiriwa kuwa anaonyesha woga katika kuipigania jamii yake na kukemea maovu katika jamii.

Pia udhaifu mwingine ni kwamba kutumia neno "eti" kwenye swala la kuvamiwa kwa clouds media kunamuweka upande wa wavamizi kwani anatilia shaka swala ambalo ni dhahiri lilitokea

By Zawadi B Lupelo/JF

Related Posts

Post a Comment