Leo Machi 2, 2017 ni siku ya Alhamisi ambapo watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii huchapisha picha na video za matukio ya nyuma ikiwa ni kujikumbusha tukio lijulikanalo kama TBT (ThrowBack Thursday).
Kwetu sisi, tunapenda kukukumbusha kwa kukuwekea picha ya Baraza la Mawaziri la mwisho la Rais wa Kwanza wa Tanzania, Julius Kambara Nyerere kabla hajang’atuka madarakani mwaka 1985.
Mwalimu Nyerere ndiye alikuwa Rais wa kwanza wa Tanzania (Tanganyika wakati huo) tangu tulipopata uhuru hadi alipotoka madarakani na kumpisha Rais Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
Wengi wa mawaziri wanaoonekana katika baraza hilo kwa sasa ni viongozi wastaafu huku baadhi wakiwa bado wanaendelea na uongozi kama Mama Anna Makinda ambaye ameteuliwa na Rais Magufuli kuwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF).
TAZAMA VIDEO MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AMUWEKA NDANI ALIYE KUWA MWENYEKITI WA MTAA................
Post a Comment
Post a Comment