const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); GWAJIMA AZUNGUMZA TENA KUHUSU UNUNUZI WA NDEGE YAKE BINAFSI - HABARI MPYA

..

GWAJIMA AZUNGUMZA TENA KUHUSU UNUNUZI WA NDEGE YAKE BINAFSI

Baada ya kimya cha muda mrefu tangu aliposema kuwa atakuja nchini na ndege yake binafsi (private jet) Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima ameibuka na kusema kwamba yupo Marekani na akirejea nchini atakuja na ndege hiyo.



Kupitia video aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, Gwajima alisema atakuja na ndege hiyo na yeyote atakayeleta ngebe, atamkata ngebe kwa jina la Yesu.

“Mimi nasema kwenye maisha yangu sishindwi. Hata ‘this time’ (muda huu) nimetoka nimekuja hapa Marekani narudi na private jet (ndege binafsi), nanunua. Wale mliopo Tanzania mnisikie, atakayeleta ngebe namkta ngebe kwa jina la Yesu,” alisema Gwajima huku akishangiliwa na umati wa watu aliokuwa akiwahubiria.

Gwajima alisema kuwa, wao kama watu wa Mungu wamepewa uwezo, nia na sababu na hivyo watafanya.

Agosti 4 mwaka huu, Gwajima alichapisha picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa amesimama mbele ya ndege hiyo na kuandika kwa kiingereza akimaanisha kuwa, karibuni ataileta ndege hiyo Tanzania kwa ajili ya kuendeleza ufalme wa Mungu. Ni wakati wa ufufuo na uzima duniani.

Siku moja baada ya Askofu Joesphat Gwajima kusema hayo, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilikana kuwa na taarifa kuhusu ujio wa ndege hiyo.

TCAA ilisema kuwa, Mtanzania yeyote anayenunua ndege nje ya nchi na kutaka kuiingiza nchini anatakiwa kwanza kuitaarifu mamlaka hiyo ili iweze kuwa na taarifa kamili. Aidha, alisema kabla ndege hiyo haijaingizwa nchini ni lazima wataalamu wa TCAA wajiridhishe kuwa wanaifamahu na ifanyiwe ukaguzi.

TCAA imesema ndege hukaguliwa kabla haijaingizwa nchini ili kujiridhisha kuwa inakidhi vigezo vya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).

Gwajima ambaye amekuwa nje ya nchi tangu Juni mwaka huu, amewataka waumini wake wakautane kanisani kwake Jumapili lakini hakusema atakuja lini.

Kila mmoja sasa anasubiria kuona kama kweli atakuja na ndege hiyo nchini.

Related Posts

Post a Comment