Mtayarishaji wa video nchini Nisher amemtaja mtu aliyesababisha bifu lake na Hanscana.
Nisher amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatano hii, kuwa baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na Khalfan ndipo Hanscana aliamua na yeye kumtengenezea bifu na kumtumia meseji nyingi za kumtukana.
“Hanscana ni kama alidandia baada ya kuona mimi na Khalfan haziivi, due to business issues akaona na yeye anitukane. Me actualy nina messages ambazo alinitumia Hanscana matusi kabisa lakini mimi nimemsamehe na naona anafanya kazi nzuri,” amesema Nisher.
Kwa sasa mtayarishaji huyo amedai kuwa tayari walishayamaliza matatizo yao na Khalfan na sasa wapo poa na kuna kazi anamsaidia kuifanya.
TAZAMA VIDEO MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AMUWEKA NDANI ALIYE KUWA MWENYEKITI WA MTAA................
Post a Comment
Post a Comment