const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); MAKETE: Afariki Dunia baada ya Kulazimishwa Kumnyonyesha Mtoto Wake - HABARI MPYA

..

MAKETE: Afariki Dunia baada ya Kulazimishwa Kumnyonyesha Mtoto Wake

Mwanamke mmoja Bi. Olida Sanga (19)amekutwa jana akiwa amekufa katika mto Luvanyina kijiji cha Isapulano kata ya Isapulano Wilayani Makete
Akizungumza na Kitulo Radiofm Mwenyekiti wa kijiji cha Isapulano mara baada za Mazishi ya Marehemu Olida,Bw. Mwatindi Mbilinyi amesema Marehemu wakati wa Uhai wake alikuwa analazimishwa kumnyonyesha mwanaye jambo ambalo huenda lilimkera na kuamua kuchukua maamuzi hayo ya kujirusha mtoni

Inaelezwa kuwa Marehemu alikuwa anaugua ugonjwa wa kifafa kwa siku nyingi
Marehemu amemwacha mwanaye Mwenye Miezi miwili wa kiume ambaye kwa sasa analelewa na Ndugu zake wa Karibu
Wananchi walianzisha jitihada za kumtafuta mnamo jumapili saa 10 jioni na kwa bahati mbaya waliopoa maiti yake kwenye mto Luvanyina hapo jana saa 5:30 asubuhi

chanzo: kitulo fm
TAZAMA VIDEO MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AMUWEKA NDANI ALIYE KUWA MWENYEKITI WA MTAA................

Related Posts

Post a Comment