const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Binti afariki akifanyiwa upasuaji kuongeza makalio! - HABARI MPYA

..

Binti afariki akifanyiwa upasuaji kuongeza makalio!

Binti wa miaka 25 amefariki baada ya upasuaji wa kuongeza makalio kwenda ndivyo sivyo, kwa mujibu wa polisi Ranika Hall kutoka Missouri Marekani amekumbwa na umauti katika kliniki ya mambo ya urembo mjini Miami ambako alikuwa anafanyiwa upasuaji.


Marehemu Ranika Hall enzi za uhai wake.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi Kliniki ambamo mama huyo alikuwa akifanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio ilipiga simu kuomba msaada majira ya saa tatu usiku siku ya alhamisi baada ya binti huyo kuonesha dalili za kushindwa kupumua. Hata hivyo dada huyo alifariki dunia saa moja baada ya kufikishwa hospitali.

Mwaka uliopita mwanamke mmoja alifariki katika kliniki hiyo hiyo na akifanyiwa upasuaji kama huu, hii imepelekea idara za polisi kuanzisha uchunguzi.


Makalio makubwa yamekuwa ni mtindo kwa miaka ya karibuni na kuwafanya wanawake wengi kuyatafuta kwa njia mbalimbali zikiwemo njia za kufanyiwa upasuaji na upandikizaji wa nyama.

Ukuaji wa teknolojia na sayansi za kimatibabu kumefanya suala la kukuza matiti na matako kuwa bei nafuu na kwa mara nyingi kufanyika bila kupoteza uhai wa mtu ingawa bado kumekuwa na mazungumzo makubwa juu ya athari zake baadae kwa mtu aliyefanya maboresho ya namna hii katika mwili wake.

Tazama video Mtoto amvua kofia Papa Francis

Related Posts

Post a Comment