const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Emoji mpya 2017 zinakujia, zifahamu mpya zinazokuja - HABARI MPYA

..

Emoji mpya 2017 zinakujia, zifahamu mpya zinazokuja


Kuna kautamaduni wa takribana kila mwaka wa tume inayosimamia ubunifu na utumiaji wa Emoji ndani ya shirika la Unicode kutambulisha emoji mpya. Kwa mwaka huu kuna mpya kadhaa.

Unicode ni shirika linalosimamia utumiaji wa teknolojia za alama mbalimbali kwenye simu na jinsi gani utumiaji wa alama hizo unafanikisha nini.

Kutakuwa na Emoji mpya 56 mpya (angawa kiujumla kutakuwa na emoji 69 – ukijumlisha na za utofauti wa jinsia).

Kikubwa zaidi ni kwamba kutakuwa na Emoji ya panzi – tena panzi aliyepata umaarufu sasa hivi kwenye mitandao ya kijamii kutokana na miguu yake….watu wakisema ni mizuri sana.


Kuna Emoji mbalimbali zilizotengenezwa zilizotengenezwa kuwakilisha wahusika mbalimbali maarufu wa filamu na stori za zamani. Hii ni pamoja na filamu maarufu ya Hulk, filamu za Aladini, Dracula, na zimwi la bahari (Mermaid).


Na pia kuna Emoji nyingi zaidi zimeongezwa za sura za tabasamu na uchokoziiii..

Baadhi ya Emoji mpya 2017


Katika kipindi chochote kuanzia sasa tegemea apps mbalimbali na simu kuja na masasisho (updates) yanayojumuisha Emoji hizi mpya.

Tazama video Mtoto amvua kofia Papa Francis

Related Posts

Post a Comment