Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mkoani Tanga wanatuhumiwa kumuua kondakta wa daladala linalofanya safari zake kati ya Nguvumali hadi Raskozone, Salim Kassim kwa kumpiga.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, kondakta huyo alifariki wakati akipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo huku chanzo cha kifo chake kikidaiwa kuwa ni kupigwa na wanajeshi hao alipoingizwa katika kambi ya jeshi.
Inadaiwa kuwa achanzo cha tukio hilo ni kondakta kumzuia mwanafunzi ambaye hakuwa amelipa nauli kutoka ndani ya daladala. Baba mzazi wa mwanafunzi huyo ni mwanajeshi kitendo kilichopelekea kondakta yule kuingizwa katika kambi ya jeshi na alipotolewa hakuwa anajitambua.
Hapa chini ni video ya mashuhuda wa tukio hilo wakielezea kwa undani zaidi.
Post a Comment
Post a Comment