const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); VIDEO: HARMONIZE AMLILIA WOLPER KWA KUMWIMBIA WIMBO AKITAKA WARUDIANE - HABARI MPYA

..

VIDEO: HARMONIZE AMLILIA WOLPER KWA KUMWIMBIA WIMBO AKITAKA WARUDIANE

Baada ya kuwa kwenye mapenzi yao kwa muda mrefu na kuachana katika hali ya usiri mkubwa mambo yamezidi kujionyesha yenyewe kuwa wawili hao ni kweli hawap0 tena pamoja.
Awali Wolper ndiye aliyeanza kusema kuwa ameachana na Harmonize lakini Harmonize hakuwa tayari kuzungumzia jambo hilo akisema yeye hafahamu kitu chochote cha zaidi habari hizo anaziona kwenye mitandao ya kijamii tu.
Wolper alianza kwa kufuta picha za Harmonize na WCB kwenye akaunti yake ya Instagram huku akiweka picha zenye maelezo kuonyesha kuwa ameumizwa.
Kwa sasa Harmonize ameonyesha kuwa ni kweli wameachana lakini bado anamuhitaji mrembo huyo kufuatia video yake inayosambaa kwenye mitandao akionekana kumuimbia Wolper wimbo wa Ibaki Story wa Rich Mavoko.
Harmonize anaimba wimbo huo huku akitaja jina la Wolper ya kuwa hataki mapenzi yao yabaki kuwa stori akimaanisha kuwa anamuhitaji waendelee.

Related Posts

Post a Comment