const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); MWASITI AWABEZA WASANII WANOENDA KUFAFANYA VIDEO ZA NYIMBO ZAO AFRIKA KUSINI - HABARI MPYA

..

MWASITI AWABEZA WASANII WANOENDA KUFAFANYA VIDEO ZA NYIMBO ZAO AFRIKA KUSINI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MWANAMUZIKI mahiri wa miondoko ya bongofleva, Mwasiti Almas "Chiti" amesema kuwa haoni sababu ya wanamuziki wa hapa nchini kwenda kufanya Video nchini Afrika Kusini wakati  hapa nchini bado tuna maandhari mazuri.

Mwasiti amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na ripota wa Globu ya Jamii juu ya maandalizi ya uandaaji wa video ya wimbo wake mpya ambao anataraji kuufanya hivi karibuni.

“nataka kufanya video wiki ijayo lakini nitafanya na mtayarishaji wa hapa ndani ambaye ni Msafiri wengi wamezoea kumwita Traveler hivyo kila mtu akae mkao wa kula kupokea nyimbo nzuri kutoka kwa Mwasiti” amema

Amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakimuambia kuwa amekaa kimya kwa muda mrefu hivyo anawaeleza kuwa amerudi na ladha ile ile ambayo imekuwa ikiishi kwa miaka mingi.



Ametaja kuwa wanamuziki wengi hapa nchini wamekuwa wakifanya muziki wa Bigijii ambao uishi kwa muda mfupi, lakini mwasiti ni habari nyingine kwani yeye asipokuwepo muziki wake bado utaishi.

Related Posts

Post a Comment