const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); UTEUZI: RAIS DKT MAGUFULI AMKUTANISHA BABA NA MWANAE BUNGENI - HABARI MPYA

..

UTEUZI: RAIS DKT MAGUFULI AMKUTANISHA BABA NA MWANAE BUNGENI


Jana Januari 16, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa viongozi watatu ambao ni wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi mmoja ambaye kituo chake cha kazi kitatajwa baadae.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa wabunge hao wawili ni Alhaji Abdallah Majura Bulembo na mwanasheria maarufu Tanzania, Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi.


Alhaji Abdallah Majura Bulembo

Abdallah Bulembo ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM anakwenda bungeni ambapo atakutana na mtoto wake, Halima Bulembo ambaye naye ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kagera kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Halima Bulembo amejizolea sifa nje na ndani ya bunge kwa kuwa ndiye mbunge mdogo kuliko wote akiwa na umri wa miaka 25.

Halima Abdallah Bulembo

Hii ni kwa mara nyingine kwa watu wenye uhusiano wa karibu kuwemo bungeni baada ya awali marehemu Dkt. Emmanuel Makaidi na mkewe Modest Makaidi kuwepo kwenye bunge la katiba mwaka 2014 lakini pia marehemu Samwel Sitta na mkewe Magreth Sitta.

Hadi sasa Rais Dkt Magufuli amefikisha idadi ya wabunge 8 wa kuteuliwa ambapo katiba ya nchi inampa mamlaka ya kuteua wabunge 10.

Uteuzi huu wa Rais Dkt Magufuli umehusishwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko katika baraza la mawaziri ambapo wananchi kwenye mitandao ya kijamii wanaamini ni suala la muda mfupi tu kabla rais hajafanya mabadiliko na kuwaingiza wabunge hawa wawili wapya.

Related Posts

Post a Comment