KAYA 10 zimekosa mahara pa kulala kaatika kijiji cha Isimike wilayani Wangingombe baada ya nyumba zake pamoja na majemo matatu ya Umma kuezuriwa na upepo mkali ulioambata na na mvua zinazo endelea kunyesha Nchi nzima kwa Uchache wake.
Licha ya kuwapo kwa Mvua chache kwa baadhi ya maeneo hapa nchini lakini wilayani Wangingombe kumetokea Mvua kubwa na kusababisha maafa na uezua nyumba za kuishi, Zahanati, na nyumba mbili za waalimu huku thamani halisi ya maafa hayo uongozi wilayani humo ukiendelea na taratibu za kufanya tathimini.
Akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka mkuu wa wilaya ya Wang’ingombe Ally Kasinge alisema kuwa kaya 10 nyumba zake zimeezuriwa mabati yake ka kukosa mahala pa kujihifadhi.
Mkuu wa mkoa wa Njombe anasema kuwa wananchi wanatakiwa kujenga nyumba imara kutokana na ukanda waliopo kuwa ni wa upepo ili kuto kubwa na majanga kama hayo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe na mbunge wa jimbo la Makambako Deo Sanga anatoa pole kwa wakazi wa kijiji hiki.
Wananchi nao wanasema walivyo adhiliwa na maafa haya huku wakitaja nyumba zao zilizofumuliwa mabati.
Post a Comment
Post a Comment