const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); TzTown Tv: Njombe Mji FC yazidi kusonga mbele yaichapa KINO BOYS - HABARI MPYA

..

TzTown Tv: Njombe Mji FC yazidi kusonga mbele yaichapa KINO BOYS


TIMU ya Njombe mji imefanikiwa kuichabanga mabao wawili kwa nunge timu ya Mamispaa ya Kinondoni KMC katika mchezo wa walio ucheza mjini Makambako katika uwanja wa Aman na kujiweka katika nafasi nzuri na kujinyakulia Pointi 21.
Timu hiyo inasema kuwa imepania kuingia Ligi kuu Tanzania na kuwa sasa inajipanga kuhakikisha kuwa inafikia katika nafasi Nzuri huku ikijinasibu kushinda mechi zake zilizo baki na kuzisaka pointi sita ili kuingia ligi kuu ya Tanzania.

Ni kelele za shangwe baada ya kufunga goli wachezaji wa Timu wa Njombe mji wanawainua mashabiki wao wakiwa nyumbani wanashangilia.

Viongozi na mashabiki wa timu ya Njombe mji wanasema kuwa walijipanga kukabiliana na mikikimikiki ya kusaga nyasi na kuzinyakua pointi zao tatu.

Kwa upande wa timu ya KMC ya jijini Dar es salaam wanasema kuwa hawakuzidiwa bali ulikuwa ni chezo mzuri lakini mbinu ziliwazidi

Related Posts

Post a Comment