Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameunda tume ya watu 12 ili kuchunguza chanzo cha moto uliotokea katika chumba kinachotumika kuhifadhia mizigo ya abiria wanaotoka nje katika Uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA) Terminal two.
Aidha Prof Makame ametoa muda wa miezi miwili kuangaliwa kwa makini utendaji wa kampuni ya Swissport.
Prof. Makame Mbarawa mapema leo hii alitembelea sehemu ya uwanja huo wa ndege na kujionea madhara yaliyosababishwa na moto uliotokea usiku wa kuamkia leo ambapo amesma kuwa mara baada ya kujua chanzo cha moto huo basi watajipanga vema ili kuhakisha madhara kama hayo hayatokei tena katika viwanja vya ndege.
Post a Comment
Post a Comment