Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amevipongeza vyombo vya habari kwa kufanya kazi nzuri ya kuelimisha jamii lakini wakati huo huo akasema kuwa kuna magazeti mawili hapa nchini yanaandika habari za kichochezi na kuwa atayafungia.
Rais Dkt Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizudua Kiwanda cha kutengeneza vinywaji cha Jambo Food Product mkoani Shinyanga ambapo alisema kuwa magazeti hayo yamekuwa yakiandika habari za uongo na hawezi kuyafumbia macho sababu amani ya nchi ipo katika hatari.
Rais Dkt Magufuli alitolea mfano wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda ambapo alisema yalitokea kuwa kuchangiwa na habari zilizokuwa zikienezwa na vyombo vya habari.
Aidha, alisisitiza kuwa sio kwamba hataki serikali ikosolewa lakini anataka ikosolewe katika kitu kilicho cha kweli. Rais Dkt Magufuli hakuyataja magazeti hayo kwa kile alichosema kuwa yanajijua.
“Hayo magazeti kila nikisema hivi, yanapindisha,siyajataji kwa sababu yanajifahamu lakini yajue kuwa siku zake zinahesabika. Serikali ninayoiongoza haiwezi kukubali amani kuvurugwa” alinukuliwa Rais Dkt Magufuli akisema.
Post a Comment
Post a Comment