Uuzaji, uzambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya ni vita inayopiganwa kwa nguvu sana, si hapa nchini tu bali duniani kote kwa sababu inapelekea kupoteza nguvu kazi kubwa sana kwani watumiaji wengi wa bidhaa hizo ni vijana.
Jeshi la Polisi Tanzania leo nimefanya mkutano na waandishi wa habari ambapo limeelezea juu ya mapambano ya dawa za kulevya na wametaja aina mbili za dawa za kulevya zinazozalishwa Tanzania ambazo ni bangi pamoja na mirungi.
Wakizungumzia kuhusu kiwango cha ulimaji wa dawa hizi za kulevya hasa bangi, Jeshi la Polisi lilitaja mikoa sita ambayo ndiyo vinara wa ulimaji wa bangi nayo ni Arusha hasa Wilaya ya Arumeru, Morogoro, Iringa, Pwani, Tanga na Mkoa wa Mara hasa wilayani Tarime.
Aidha, Polisi wametoa pongezi kwa Wakuu wa Wilaya kwa mchango wao mkubwa ambao wameuonyesha katika kupiga vita dawa hizi hasa wilayani Tarime ambapo viongozi wa serikali za mitaa wamepewa jukumu la kuhakikisha eneo analoliongoza hakuna hata mche mmoja wa bangi.
Kwa upande wa mirungi, mikoa miwili inayoongoza kwa kulima dawa hiyo ni Kilimanjaro hasa Wilaya ya Same na Mkoa wa Arusha.
Post a Comment
Post a Comment