Saraha akiwa na Fundi Samweli
Akiwa kwenye kipindi cha FNL ya EATV, mwanadada huyo ambaye anaipeperusha vilivyo Tanzania nchini Sweden kupitia ngoma zake anazoimba kwa Kiswahili, amesema sababu kubwa ya kutengana na Fundi Samweli ni aina ya kazi wanazofanya huku akisema kuwa ni jambo gumu kwa watu wawili wanaofanya kazi za aina hiyo kudumu katika mahusiano ya kimapenzi.
Saraha ambaye hakutaka kuingia kwa undani kwenye kiini cha kutengana kwao, amesema kabla ya kutengana kabisa walikuwa wakifanya kazi pekee bila masuala ya mapenzi lakini ilifikia hatua wakaamua kukubaliana kuwa mbali kabisa huku akisema kuwa kwa sasa hawafanyi tena kazi pamoja na hata mawasiliano si ya mara kwa mara.
"Mimi na Fundi Samweli tuliweka pembeni mapenzi, tuliona kwa kazi tunazofanya mapenzi hayawezekani, halafu tulikuwa bize sana na kazi muda mwingi ilikuwa ngumu kuendelea, kwa sasa huwa tunawasiliana mara chache kwa ajili ya kazi, lakini najua ana bendi yake, yeye ana mambo yake na mimi nina mambo yangu, namtakia kila la kheri" Alisema Saraha.
Katika hatua nyingine Saraha amekiri kuwa na mpenzi mwingine kwa sasa huku akigoma kumuweka wazi.
Saraha ni binti wa kizungu ambaye anaimba bongo fleva kwa lugha ya Kiswahili, na producer wake mkuu alikuwa ni Fundi Samweli ambaye ndiye aliyekuwa mchumba wake huku akitamba na ngoma kama vile Kwasakwasa na kuahidi kutoa ngoma nyingine na Fid Q na Big Jahman
Post a Comment
Post a Comment