Shirika la ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), limesema kukatika kwa umeme kila wakati kunasababishwa na uboreshaji wa miundombinu katika maeneo mbalimbali husika, hususani katika Jiji la Dar es Salaam.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji, alisema suala la kukatika kwa umeme linatokana na kuboreshwa kwa miundombinu ya umeme kwa kuweka mipya.
“Lakini pamoja na maboresho hayo, kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara, kama shirika huwa tunaomba radhi kwa wananchi kabla ya kukata ingawa tatizo hilo linakuwa nje ya uwezo wetu,” alisema Laila.
Alisema hata hivyo kabla ya kukata umeme, shirika hutoa taarifa kwa umma kwa njia mbalimbali ikiwemo matangazo kupitia vyombo vya habari nchini.
– MTANZANIA
Post a Comment
Post a Comment