Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa nyumbani kwake Chato Mkoani Geita jana alipata wasaa wa kutembelea Shule ya Msingi Chato aliposoma elimu yake ya msingi (Darasa la kwanza hadi la saba) na kuzungumza na walimu pamoja na wananfunzi. Rais Dkt Magufuli aliahidi kuwajengea madarasa matatu na ofisi moja ya walimu.
Lakini pia Rais Dkt Magufuli alitembelea kibanda kimoja cha kusafishia viatu (Shoeshine) kilichopo eneo la Stand ya zamani Chato ambapo alipiga stori na aliowakuta katika kibanda hicho. Kabla ya kuwa rais alikuwa akisafishia viatu vyake katika kibanda hicho alipokuwa yupo mapumzikoni.
Lakini Rais Dkt Magufuli pia alikumbukia walivyokuwa wakikaa hapo na kula karanga kipindi cha nyuma hivyo akaamua kununua karanga na kuanza kula pamoja na waliokuwepo hapo. Hapa chini ni video ya Rais Dkt Magufuli akiwa katika kibanda hicho.
Post a Comment
Post a Comment