Januari 8, 2017 aliyekuwa Rais Mteule wa Ghana, Nana Akufo-Addo alikula kiapo kuwa Rais wa Ghana baada ya kumshinda mpinzani wake ambaye ndiye alikuwa rais kwa wakati huo John Mahama.
Watu wengi wamevutiwa na namna siasa za Ghana zinavyoendeshwa ambapo baada ya kiongozi wa upinzani kushinda uchaguzi makabidhiano ya ofisi yamekwenda vizuri pasi na kuwepo vikwazo vya aina yoyote.
Baada ya kuapishwa kuwa Rais, Nana Akufo-Addo alipata nafasi ya kukutana na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani Afrika ambapo miongoni mwao alikuwamo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kutoka Tanzania na Kizza Besigye kutoka nchini Uganda.
Haikufahamika mara moja kwenye kikao hicho walizungumza nini lakini inaaminika kuwa ni namna ya kuimarisha vyama vya upinzani na hatimaye kuweza kushika dola kama ilivyokuwa kwa Ghana.
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo (kushoto) akiwakaribisha viongozi kutoka nchi za Tanzania na Uganda, Freeman Mbowe (katikati) na Kizzya Besigye (kulia) kwa ajili ya kikao kilichofanyika Ikulu ya nchi hiyo Jumatatu jioni. Viongozi hao walikuwa miongoni mwa wageni walioalikwa kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais Nana Akufo, Januari 8, mjini Accra, Ghana
Post a Comment
Post a Comment