Wanasheria wanaowawakilisha raia wawili wa Irak wenye kibali cha kuingia nchini Marekani waliokuwa wanashirikiana na jeshi la nchi hiyo wamefungua mashitaka dhidi ya Rais Donald Trump na serikali ya Marekani baada ya kuwekwa kizuizini uwanja wa ndege mara tu baada ya kuingia Marekani siku ya Ijumaa.
Kesi hii dhidi ya serikali inamaanisha ni tukio la kwanza la kisheria dhidi ya amri zenye utata zinazotolewa na rais wa wa nchi hiyo ambayo moja kwa moja haitambui uwepo wa wakimbizi wa Syria waliopo nchni humo kwa sababu za machafuko ya kisiasa nchini mwao, na pia inazuia wakimbizi wengine kutoingia nchini Marekani kwa kutekeleza kile ambacho Rais amekiita “kumchunguza kila mhamiaji” aliyepo na anayetaka kuingia nchini Marekani.
Kwa mujibu wa vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani, watu hao wawili waliruhusiwa kisheria kuingia nchini Marekani lakini wakawekwa kizuizini kutokana na amri ya Trump kusitisha safari zote kutoka na kwenda nchi kadhaa zenye waumini wengi wa kiislamu
Mmoja wa watu hao, Hameed Khalid Darweesh, aliajiriwa na jeshi la Marekani wakati wa vita nchini akifanya kazi ya ukalimani, aliachiwa kutoka kizuizini mchana wa Jumamosi.
“Marekani ni nchi inayothamini uhuru,” Darweesh aliwaambia waandishi wa habari muda mfupu baada ya kuachiwa kwake katika uwanja wa ndege. “Marekani ni taifa kubwa kuliko mataifa yote duniani.”
Alipoulizwa kuhusu Trump, Darweesh alisema, “Nampenda, ila kwa sas nina wasiwasi.”
Mtu wa pili ni Alshawi, aliyepewa kibali mwanzo wa mwezi huu akiwa na lengo la kuwatembelea mke pamoja na mtoto wake ambao walishapewa kibali cha ukimbizi kwa sababu ya mchango wa mkewe kwa jeshi la Marekani.
Wanasheria wa watu hawa raia wa Irak wameiomba Mahakama isikilize kesi yao kwakuwa kumuweka kizuizini mtu mwenye kibali ni kinyume cha sheria.
Post a Comment
Post a Comment