const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); PICHA: VIJANA WAWILI WAWEKA REKONDI KWA KUFUNGA NDOA YA BEI RAHISI - HABARI MPYA

..

PICHA: VIJANA WAWILI WAWEKA REKONDI KWA KUFUNGA NDOA YA BEI RAHISI



Vijana wawili wapenzi ambao stori yao kuhusu ndoa ya bei rahisi waliyofunga ilizua hisia za watu wengi kwenye mitandao ya kijamii, sasa wameahidiwa kulipiwa gharama zote za mapumziko baanda ya ndoa (honeymoon).
Wilson Mutara (26) na Ann Wambui (24) kutoka nchini Kenya inaripotiwa kuwa walifunga ndoa kwa gharama ya Ksh 100 ambayo ni sawa na TZS 2,147 ambapo gharama hizo zilikuwa kwa ajili ya kununua pete tu.
Ndoa hiyo iliyotajwa kuwa ya bei rahisi kuwahi kutokea nchini humo haikua na sherehe baada ya wawili hao kutoka kanisani na walivalia fulana walipokwenda kufunga ndoa.

“Tulikwenda nyumbani tukapika ugali na sukuma wiki, tukala na tukalala. Hakuna kitu cha kipekee tulichokifanya katika mapumziko (honeymoon) yetu” alisema Mutura.

Padri aliyefungisha ndoa hiyo alichapisha habari hiyo na ndipo mwakilishi wa Kampuni ya Utalii ya Bonfire Adventure alipokutana na wanandoa hao.


Kampuni hiyo ndiyo ilijitolea kudhamini mapumziko ya wawili hao baada ya kufunga ndoa.

Related Posts

Post a Comment