const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); MWANAFUNZI WA CHUO AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HABARI YA UONGO WHATSAPP KUHUSU MBUNGE LEMA - HABARI MPYA

..

MWANAFUNZI WA CHUO AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HABARI YA UONGO WHATSAPP KUHUSU MBUNGE LEMA




Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam (ARU) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupandishwa kizimbani akikabiliwa na tuhuma ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa WhatsApp.

Juvenal Shirima (25) anayedaiwa kuwa ni Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anatuhumiwa kutenda kosa hilo Januari 3 mwaka huu.

Wakili wa Serikali, Adolf Mkini akimsomea hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa alidai kuwa mshtakiwa huyo kupitia kundi la mtandao wa WhatsApp la Lowassa Foundation and Bunge Live alichapisha habari ya uongo iliyokuwa ikisomeka “Nimepata rehema ya mipango michafu sana iliyokuwa inapangwa na bado inapangwa dhidi ya uhai wa (Mb), Godbless Lema…”
Mshatakiwa huyo alikana shtaka hilo na aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya TZS milioni 2 kila mmoja pamoja na barua.

Related Posts

Post a Comment