Kupitia mitandao ya kijamii imesambaa video ikionyesha kundi la wanaume wakishirikiana kumchapa viboko mwanamke mmoja ambaye hakufahamika mara moja alikosa nini.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi wala wizara yenye dhamana zinadai kuwa tukio hilo limetokea Kijiji cha Nyasurura, Serengeti mkoani Mara.
Katika video hiyo, wanaonekana wanaume ambao wapo kwenye mkusanyiko kama vile mkutano huku wakiwa wameshika fimbo na kumchapa mwanamke huyo kwa zamu.
Wizara ya Afya, pamoja na Jeshi la Polisi tayari zimanza uchunguzi kufahamu kwanza kama tukio hilo limetokea nchini Tanzania, na kama ni Tanzania ni sehemu gani ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi.
Itazame video hiyo hapa chini;
WANAUME WAKISHIRIKIANA KUMCHAPA VIBOKO MWANAMKE MMOJA TUKIO LINALODAIWA KUTOKEA SERENGETI MKOANI MARA.
Post a Comment
Post a Comment