const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); NCHI SABA (AFRIKA & ASIA) AMBAZO RAIS TRUMP HATAKI RAIA WAKE WAINGIE MAREKANI - HABARI MPYA

..

NCHI SABA (AFRIKA & ASIA) AMBAZO RAIS TRUMP HATAKI RAIA WAKE WAINGIE MAREKANI

Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajia kusaini amri itakayoweka mazingira magumu kwa raia kutoka baadhi ya nchini za Mashariki ya Kati na Afrika kupewa visa ya kuweza kuingia nchini Marekani.

Rais Trump amefikia hatua hiyo kwa kile alichosema ni kuimarisha ulinzi na usalama wa raia wa Marekani pamoja na mali zao.

Nchi saba zitakazoathirika zaidi na amri hii ya Rais Trump ni zile zenye waislamu wengi ambazo ni Syria, Iran, Iraq, Libya, Yemen, Sudan, na Somalia.

Rais Trump ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba leo itakuwa siku muhimu sana kwa usalama wa taifa la Marekani ambapo baadae leo anatarajia kutembelea Makao Makuu ya Usalama wa Ndani ikiwa ni jitihada za kuimarisha ulinzi.


Wakati wa kampeni zake pia Trump aliahidi kuwa atajenga ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico ili kuzuia raia wa Mexico wanaoingiza dawa za kulevya ambapo wengine huingia na kuanza kuwa vibaka na wabakaji.

Aidha imeelezwa kuwa kutakuwa na ukaguzi mkali utakuwa ukifanyika kwa raia watakaokuwa wanaingia Marekani ili kuzuia raia wa mataifa saba ya Afrika na kutoka eneo la Mashariki ya Kati yote yalio na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu.

Mashirika ya haki za kibinadamu yamekuwa yakikosoa misimamo mikali ya Trump dhidi ya waislamu ambapo mara nyingi amekuwa akiwahusisha na ugaidi. Katiba ya Marekani inapiga marufuku ubaguzi wa kidini lakini inasemekani huenda Trump akaibadilisha kwa madai ni hatua za dharura za kuimarisha usalama.

Related Posts

Post a Comment