const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); MRADI WA UMWAGILIAJI NI JIPU DODOMA - HABARI MPYA

..

MRADI WA UMWAGILIAJI NI JIPU DODOMA



Mradi ulitakiwa kukamilika ndani ya miezi minne, hadi sasa ni miaka sita na haujakamilika bado.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeshangazwa na mradi wa umwagiliaji kwa njia ya matone katika kijiji cha Gawaye mjini Dodoma kuchukua zaidi ya miaka sita bila kukamilika badala ya miezi minne iliyokuwa imepangwa kabla ya kuanza kwa mradi huo wa zaidi ya shilingi milioni 800.

Kamati hiyo ilishangazwa kwakuwa kazi zilizofanyika ni tofauti na zilizoainishwa kwenye mkataba. Mfano ni matumizi ya zaidi ya shilingi milioni 200 kununua mbolea na miche, vitu vilivyopaswa kufanywa na wananchi wanaoshiriki mradi huo.

Mbunge wa Rombo, Mh. Joseph Selasini alishangazwa kwa zaidi ya shilingi milioni 190 kutumika kununua mbolea ya samadi kwa ajili ya miche ya zabibu wakati mbolea hiyo inapatikana kwa wingi maeneo hayo. Katika maandiko ya mradi huo, haikutakiwa kununuliwa mbolea na miche bali wananchi wanaoshiriki mradi huu walitakiwa kufanya kwa nguvu zao.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Vedasto Ngombale alisema walichokibaini ni kuwa mradi umetekelezwa kinyume na mkataba unavyotaka kwani wananchi hawajatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa mkataba. Uongozi wa Chama cha Ushirika umesema matamko ya kisiasa ndio yaliyokwamishwa mradi huo kwakuwa wanachama hao waliambiwa watapewa mikopo ambayo hawajapatiwa, jambo lililowapa shida katika utekelezaji.

Related Posts

Post a Comment