const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); MWAKYEMBE ANYOOSHA MAELEZO KUHUSU UTEUZI WA MAMA KILANGO - HABARI MPYA

..

MWAKYEMBE ANYOOSHA MAELEZO KUHUSU UTEUZI WA MAMA KILANGO


Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe ametole ufafanuzi kuhusu uteuzi wa mama Anne Kilango Malecela kuwa Mbunge kwa kusema jambo hilo limekuwa likiripotiwa au kusemwa tofauti kwenye magazeti na mitandao ya kijamii tofauti na uhalisia wake kisheria na kikatiba.

Kumekuwa na mjadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya Rais Dkt. John Magufuli kumteua mama Kilango kuwa Mbunge kwamba Rais amevunja Katiba kwa vigezo viwili; kwanza kwa kumteua ubunge wakati alimtumbua alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na pili Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamtaka Rais kuteua wabunge kumi ambapo angalau watano kati yao wanatakiwa kuwa wanawake.

Waziri Mwakyembe alitoa ufafanuzi alipokuwa anazungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu Iringa kwamba; “Sioni tatizo la kisheria wala kikatiba alilovunja Rais kumteua Kilango kuwa Mbunge kwa sababu siku anamuondoa kwenye nafasi ya Mkuu wa Mkoa alisema atampangia kazi nyingine, na kazi nyingine ameona amteue kuwa Mbunge.”

Akifafanua kuhusu mamlaka ya Rais kuteua wabunge kumi, alisema kuwa hoja inayojengwa na watu kwamba Rais amevunja Katiba katika uteuzi wa wabunge kwa madai kuwa atakapokuwa amemaliza uteuzi kutakuwa na wabunge wanaume sita na wanawake wane wakati wanatakiwa kuwa sawa, ni hoja dhaifu.

Alisema ibara ya 66, ibara ndogo ya kwanza A inasema kitu tofauti na kile wanachokisema watu. “Kama hicho kipengele kingekuwa kinaeleza kuwa wabunge kumi maana yake inamfunga na kumlazimisha Rais kuteua wabunge kumi, lakini kipengele hicho kinasema “wabunge wasiozidi kumi” ikimaanisha akitaka anaweza kuteua wabunge chini ya hapo (si lazima kufikisha idadi yote ya wabunge kumi anaoruhusiwa kuwateua). Pia alieleza kuwa kipengele hicho cha Katiba kinaposema kuwa kati ya hao wabunge kumi angalau watano wawe wanawake ni vitu viwili tofauti na kama kingesema kati ya hao kumi watano wawe wanawake.

Related Posts

Post a Comment