Doto Cosmas, miongoni mwa wachimba madini walionasa kwa kuporomoka kwa kifusi katika mgodi wa dhahabu RZ mkoani Geita kilichowafanya wabaki ardhini kwa siku tano bila kupata huduma yoyote muhimu kwa binadamu.
Juhudi za wataalamu wa uokoaji zilionesha kuleta mafanikio baada ya mara ya kwanza kufanikiwa kuwapatia wachimbaji hao walionasa tochi, kalamu na karatasi ili waandike mahitaji yao ya muhimu wanayotka wafikishiwe ndani ya muda mfupi ambapo kijani Doto aliandika apatiwe sigara na kiberiti. “Niliona niwaombe wanipatie sigara kabla ya chakula nikihofia kula kwa pupa na kuwa na madhara kwangu kutokana na kukaa muda mrefu bila kula,” alisema.
“Nilipata matumaini mapya ya kuishi tena baada ya kuonja kifo. Niliona raha ya matumaini hayo ni kupewa sigara,” aliongeza zaidi Doto. Hata hivyo ombi hili halikuweza kutimizwa kwakuwa sehemu waliyokuwamo kulikuwa na mabomba yanayopitisha hewa inayowasaidia kupumua (oksijeni), hivyo kuwasha sigara kungeweza kupelekea hatari ya kuanzisha milipuko utakaowaua mara moja.
Post a Comment
Post a Comment