const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); BREAKING: WACHIMBAJI WALIOFUKIWA NA KIFUSI GEITA WASEMA WAPO HAI, WATUMA MAJINA YAO - HABARI MPYA

..

BREAKING: WACHIMBAJI WALIOFUKIWA NA KIFUSI GEITA WASEMA WAPO HAI, WATUMA MAJINA YAO


Wachimbaji waliofukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ Nyarugusu mkoani Geita wametuma taarifa kwa waokoaji kuwa wapo 15 na kwamba wote wapo hai.

Wachimbaji hao ambapo bado hawajaokolewa wamesema kuwa mmoja wao amejeruhiwa ila wengine ni wazima wakiomba kuteremshiwa soda, maji na sigara.


Awali iliripotiwa kuwa walikuwa 14 ambapo ni watanzania 13 na raia mmoja wa China lakini kwa taarifa hii mpya inaonyesha kuwa wapo 15.

Wachimbaji hao walifukiwa tangu juzi ambapo shughuli za uokoaji zinaendelea wakiwa bado hawajapatikana.

Related Posts

Post a Comment