Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini China walicharuka na kukasirishwa na kitendo cha kikatili alichofanyiwa panya mmoja aliyekamatwa na kuuawa baada ya kula mchele dukani. Baada ya kumuua panya huyo, wafanyakati katika duka hilo lililopo Zhuhai jijini Guangdong walimning’iniza kwa kumfunga kamba na kumuwekea bango lililosomeka “Sitarudia tena kufanya hivi.”
Bango linalosomeka “Sitarudia tena kufanya hivi” alibandikiwa panya huyu aliyeuawa kwa kula mchele
Lai Haiwen, mtu aliyepiga na kupost picha hiyo, aliiambia CNN kuwa haoni kwanini watu wanakuwa wanafiki kwani nchini humo kuna Tamasha la “Nyama Choma” lijulikanalo kama Yulin Dog-meat Festival linalofanyika kila mwaka ambapo mbwa zaidi ya 10,000 huuliwa na kuwa msosi wa watu, kwahiyo anashangaa watu kuwa wakali kuhusu panya – aliyeiba mchele.
Lakini zaidi ya watu 6,000 waliochangia kwenye post hiyo iliyosambaa nchini China walikasirishwa na kitendo hicho walichokiita “cha kikatili.”
“Mnaweza kumuua (panya), lakini sio kumtesa. Ingawa panya wana madhara, lakini tuheshimu uhali.” Aliandika mchangiaji mmoja.
Mwengine aliandika: “Kila kiumbe hai kinatakiwa kina maisha yake, kwanini tumtese panya? Kama wewe ungekuwa ni panya, je usingeona kuning’inizwa baada ya kuuliwa ni kitendo cha kikatili? Kuiba mchele ni moja ya asili ya uharibifu wa panya. Anafanya hivyo ile aweze kula na kuendelea kuishi.”
Post a Comment
Post a Comment