const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); BIASHARA: BENKI ZIKILIA HALI NGUMU, MITANDAO YA SIMU YAWEKA REKODI YA FAIDA - HABARI MPYA

..

BIASHARA: BENKI ZIKILIA HALI NGUMU, MITANDAO YA SIMU YAWEKA REKODI YA FAIDA




Kuelekea mwisho wa mwaka 2016 mabenki 14 hapa nchni yalitangaza kupata hasira kutokana na kupungua kwa miamala ya fedha inayofanyika na benki hizo kitendo kilichopelekea Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuchukua umiliki wa benki ya Twiga Bancorp Ltd.

Benki Kuu ilifikia hatua hiyo kutokana upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na sheria ya mabenki na taasisi za fedha nchini.


Kama watu hawafanyi miamala ya kifedha benki, pesa zao zipo wapi?

Jibu la swali hili linapatikana tukiagalia wapinzani wakubwa wa mabenki katika kufanya miamala ya kifedha ambao ni kampuni za simu za mkononi.

Katika miezi miwili ya Novemba na Disemba mwaka jana (kipindi ambacho benki hizi zilitangaza hasara) makampuni ya simu za mkononi yaliingiza faida ya shilingi trilioni 13 kupitia miamala ya huduma za fedha.

Kaimu Meneja Habari wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala amesema faida hiyo imepatikana kutokana na ongezeko kubwa la matumizi ya huduma za fedha kupitia mitandao ya simu.

Kampuni zilizohusika na miamala hii ni Airtel, Halote, Tigo, VodaCom na Zantel

Related Posts

Post a Comment