Uongozi: “Nitafanya mabadiliko. Mfano mzuri nilipotembelea Shirika la Reli Tanzania, nako pia kulikuwa na tatizo kama hilo lakini baada ya kuulizwa kiundani nikaambiwa tatizo ni uongozi na si fedha, nitaleta kiongozi ambaye haijui Posta kabisa. Nafikiri huyo anaweza kuiongoza vizuri kuliko akipewa madaraka mtu ambaye anaifahamu.” Alisema Profesa Mbarawa.
Kuhusu mishahara: Kuna tatizo la wafanyakazi kutolipwa mishahara yao jambo ambalo Mkurugenzi wa Shirika alishindwa kulitolea majibu. Hii imekuwa ni sababu kwa baadhi ya wafanya kazi kutofanya kazi zao – kigezo ikiwa ni kutolipwa mishahara yao.
Wafanyakazi: “nitawanyoosha wafanyakazi wote wanaozembea kufanya kazi kama nilivyofanya katika makampuni mengine. Baada ya matembezi ya ofisi zote za posta nimejua kuwa wafanyakazi ni wengi sana lakini nimewakuta wateja 20 tu, je wafanyakazi wengine mnafanya nini? Aliongeza.
Post a Comment
Post a Comment