Ndege ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) iliyokuwa ikitoka Mwanza kwenda Dar es salaam jana ililazimika kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza dakika ishirini baada ya kuanza safari yake.
Ndege hiyo iliyoruka kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza kwa safari ya kuelekea Dar es salaam saa mbili asubuhi, ililazimika kutua kwa dharura uwanjani hapo dakika 20 baadae kwa ajili ya kurekebisha dharura ambayo mpaka muda huo ilikuwa haijafahamika.
Rubani aliwataarifu abiria kuwa wanalazimika kutua uwanjani hapo kwa sababu ya dharura iliyojitokeza. Baada ya wataalamu kuikagua ndege hiyo waligundua mlango wa sehemu ya kuwekea mizigo haukufungwa vizuri, kitu kilichosababisha kuwaka kwa taa ya tahadhari iliyomlazimu rubani kuishusha ndege hiyo.
-Mtanzania
Post a Comment
Post a Comment