const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); ASKARI AJIUA KISA WIVU WA MAPENZI, ‘MCHEPUKO’ WATAJWA KUWA CHANZO - HABARI MPYA

..

ASKARI AJIUA KISA WIVU WA MAPENZI, ‘MCHEPUKO’ WATAJWA KUWA CHANZO

Askari wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania aliyekuwa akifanyakazi Kituo Kidogo cha Polisi katika Tarafa ya Igurubi wilayani Igunga mkoani Tabora, amejiua kwa kujinyonga kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Askari huyo aliyefahamika kwa jina la G.4185 PC Geofrey Mwenda (32 ) inadaiwa kuwa alijiua kwa kujinyonga na kanga kwenye mti baada ya kugundua hawara yake ana mwanaume mwingine.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora akithibitisha kutokea kwa tukio hili alisema kuwa lilitokea juzi saa tatu usiku ambapo mke wa marehemu alikuwa amesafiri ndipo marehemu akaamua kutafuta mwanamke mwingine (jina lake halikutajwa).

Baada ya muda mfupi marehemu alikuja kugundua kuwa mpenzi wake wa nje ya ndoa (mchepuko) ana mwanaume mwingine tofauti na yeye kitu kilichomkwaza sana na kuamua kujiua.

Related Posts

Post a Comment