const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); YAJUE MAMBO 37 MUHIMU UTAYOWEZA JUTIA UKIZEEKA - HABARI MPYA

..

YAJUE MAMBO 37 MUHIMU UTAYOWEZA JUTIA UKIZEEKA


Yafuatayo ni mambo 37 utayoyajutia zaidi uzeeni kwako.

1. Kutosafiri ulipokuwa na nafasi ya kufanya hivyo: Huwa ni vigumu zaidi kupata nafasi ya kusafiri umri unavyozidi kusonga mbele, hasa ukiwa na familia na mahitaji ya kulipia gharama za watu watatu au zaidi badala ya kujilipia wewe mwenyewe.

2. Kutojifunza Lugha Nyengine: Utajilaumu sana ukija kugundua kuwa ulipokuwa chuoni ulitumia miaka mitatu kujifunza lugha nyengine lakini sasa haukumbuki hata kidogo.

3. Kuendelea kubaki kwenye mahusiano mabaya ya kimapenzi: Kila aliyewahi kutoka kwenye mahusiano mabaya ambaye akikumbuka yaliyokuwa yakimkuta na hutamani kuwa angeachana na mahusiano hayo mapema zaidi.

4. Kukaa juani muda mrefu: Mikunjo usoni (ndita), na kansa ya ngozi kwa kiasi kikubwa huweza kuepukwa kama ukijilinda. Unaweza kutumia mafuta ya nazi kufanikisha hili!

5. Kukosa nafasi ya kwenda kumuona mwanamuziki unayempenda zaidi: Wengine wakisikia mwanamuziki wanaempenda zaidi amekuja nchini au kwenye mji wake husema “Nitakwenda kwenye tamasha siku nyengine wakija tena.” Na mara nyingi nafasi kama hii inaweza isijirudie.

6. Woga wa kufanya vitu: Miaka ya baadae ukija kutafakari maisha yako utakuwa ukijiuliza ni nini kilichokuwa kikikuogopesha?

7. Kutoipa kipaumbele afya yako ya mwili: Katika kipindi ambacho mwili una nguvu kufanya mambo mengi, wengi wetu huutumia muda huo kwenye makochi tukiwa hatufanyi mambo ya maana kimaisha. Ukishatimiza miaka 40, 50, 60, na zaidi, utajilaumu ukifikiria mambo ambayo ungeweza kuyafanya.

8. Kukubali jinsia yako ikuchagulie unaloweza / usiloweza kulifanya: Vitu vichache sana duniani vinaweza kufikia ubaya wa kumsikia mzee akisema, “Sikia nikwambie, enzi zile ilikuwa huwezi kufanya kitu kama hicho.”

9. Kutoacha kazi mbaya: Tambua kitu kimoja, ni kweli kwamba unatakiwa kulipia gharama za maisha yako, lakini kama hujaweka mipango kuiboresha hali yako uliyonayo sasa utakuja kushtuka umekaa “motoni” kwa zaidi ya miaka 40.

10. Kutoongeza bidii ulipokuwa shuleni: Sio tu kwamba alama zako za ufaulu zina nafasi kubwa ya wapi utakuwa maishani. Bila shaka lazima utakuja kuwaza ungerudishwa shule kwa sasa ungeweka jitihada na kuzingatia kwa kiasi gani.

11. Kutotambua ulikuwa mzuri kiasi gani: Wengi wetu tunakuwa hatuna furaha ujanani kwa muonekano wetu, lakini ukweli ni kwamba, ujanani ndio kipindi ambacho uzuri wa mtu unakuwa katika kiwango chake cha juu kabisa ukilinganisha na kipindi chochote kile maishani mwako.

12. Kuogopa kusema “Nakupenda.” : Unapozidi kuwa mtu mzima, hujali kwamba mtu uliyempenda hakukupenda pia — ila unajali kwamba ulishamwambia mtu huyo hisia zako kwake.

13. Kutosikiliza ushauri wa wazazi wako: Hutaki kusikia wanachokwambia ukiwa mdogo, lakini ukweli usiopingika ni kwamba mambo mengi ambayo wazazi wako wanasema kuhusu maisha ni ya kweli.

14. Kuwa na ubinafsi ujanani: Kikweli lazima utakuja kujisikia aibu kwa kuwahi kuwa na tabia hii.

15. Kujali sana yanayosemwa na wengine: Ukweli ni kwamba miaka 20 baada ya sasa hutajali chochote kuhusu watuambao mwanzo ulijali sana watakachosema kuhusu wewe.

16. Kutimiza ndoto za wengine badala ya zako mwenyewe: Kusaidia watu wengine ni jambo zuri sana, lakini sio pale inapomaanisha kuwa wewe hautang’ara tena.

17. Kutopata maendeleo kwa kasi ya kutosha: Mara nyingi wazee wakifikiria kuhusu yalivyokuwa maisha yao hasa katika kipindi walichokuwa wakijivuta vuta kufanya mambo ya maana na kujuta kuwa huu ni muda ambao waliupoteza.

18. Kubaki na kinyongo, hasa kwa wale unaowapenda: Yanini kila siku ubaki na hasira kuhusu jambo moja tu? Kubali yaishe na maisha yaendelee.

19. Kukubali kuburuzwa buruzwa: Watu wazima hawakubali upuuzi wowote kutoka kwa mtu yoyote. Wewe pia unatakiwa kuwa hivi.

20. Kutofanya shughuli za kujitolea: Bila shaka unaweza kutojuta kwa kutojitolea, lakini unapozidi kukaribia mwisho wa maisha yako na ukikumbuka kuwa hujatoa mchango wako kuifanya jamii yako au dunia kuwa bora zaidi ni jambo linalowahuzunisha wengi.

21. Kutozingatia afya ya meno yako: Sugua, ng’arisha na kumuona daktari wa meno mara kwa mara. Utakuja kuona kuwa lilikuwa jambo rahisi sana kwa wewe kulifanya pale utakapokuwa na mapengo.

22. Kutowauliza babu na bibi yako maswali wakati wa uhai wao: wengi wetu hujua mwishoni kabisa kwamba wazee wetu wana mengi ya kutufunza na kutueleza. Wanaweza kukuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kinakusumbua kuhusu maisha yako ya nyuma, lakini ni mpaka uwaulize – katika uhai wao.

23. Kutumia muda mwingi kufanya kazi: Wakati wa kufariki, hakuna hata mmoja wetu atakayetamani kwamba angeendelea kutumia muda mrefu zaidi akiwa ofisini, lakini wote wanatamani wangetumua muda mwingi zaidi wakiwa na familia zao, marafiki pamoja na kufanya mambo wanayopenda.

24. Kutojifunza kupika chakula unachokipenda: Kujua kupika chakula ukipendacho zaidi kunafanya hata mitoko yako ya sherehe na ile ya chakula cha jioni iwe na maana zaidi kwako.

25. Kutotafakari maisha yako yanavyokwenda: Vijana mara nyingi wapo bize muda wote, lakini mara nyengine kukaa na kutafakari kila kinachotokea ni jambo jema zaidi.

26. Kutomaliza yale unayoyaanzisha: Kushindwa kumalizia yale unayoanzishwa ni janga. Utakuja kujikuta ukisema, “Nilikuwa na ndoto ya kuwa Daktari. Na nilishajaza mpaka fomu za kujiunga na masomo, lakini…”

27. Kutokuwa na jambo hata moja litalofanya ukumbukwe kwenye sherehe: Utakwenda kwenye sherehe nyingi sana maishani mwako. Huoni kwamba utajisikia vizuri sana uwepo wako ni wa muhimu katika sherehe hizo?

28. Kukubali jamii yako iongoze maisha yako: Kukubali matarajio ya jamii kwako ndio yaendeshe maisha yako si jambo jema sana. Usikubali wakwambie, “Sisi huwa hatufanyi hilo.”

29. Kukubali urafiki kuingilia hatma ya maisha yako: Umri unavyozidi kusonga mbele, marafiki wanatengana. Kung’ang’ania yaliyopita badala ya kukubali kwamba mambo yamebadilika huweza kuwa sababu ya manung’uniko yasiyokwisha.

30. Kutocheza na wanao kwa muda wa kutosha: Ukishakuwa mzee utagundua kuwa mwanao alitamani kucheza na wewe na sasa hakutaki hata chumbani kwake akifumbua macho yake.

31. Kutojitoa muhanga (hasa kwenye mapenzi): Kujua kwamba ulifanya jambo kwa imani tu, japo mara moja — hata kama ukaja kuangukia pua — ni jambo litalokupa faraja sana ukiwa mzee.

32. Kutofanya juhudi za makusudi kuwa na marafiki wapya: Kutengeneza mafariki yaweza kuonekana jambo la kipuuzi ujanani, lakini baadae kupitia urafiki huo huo ndio inaonekana nafasi za kazi zinapatikana kirahisi zaidi.

33. Kuwa na woga kupita kiasi: Kama mwanamuziki Tom Petty alivyoimba, “Vitu vingi ninavyoogopa hata havitakuja kutokea.”

34. Kukutwa ukifanya upuuzi usio wa lazima: Ni nani anayehitaji fedheha za namna hii?

35. Kutotumia muda wa kutosha na unaowapenda: Kutotumia muda wa kutosha na uwapendao – ni mbaya. Muda tunaotumia tukiwa na tuwapendao ni wa thamani kubwa.

36. Kutofanya maonesho mbele ya kadamnasi: Jambo hili halileti majuto kwa walio wengi, lakini wazee wengi wanatamani wangejua — japo mara moja tu — unajisikiaje kusimama mbele ya watu na kuonesha kipaji chako.

37. Kutoshukuru mapema: Yaweza kuwa ngumu sana kuona mwanzoni, lakini hujidhihirisha kuwa kila wakati katika dunia hii — toka vitu vidogo mpaka vile vya kushangaza sana — ni zawadi ambayo sisi sote tuna bahati kubwa sana kuiishi.

Related Posts

Post a Comment