const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); ASHTAKIWA KWA KUENDESHA GARI KICHWA KIKIWA KIMEPITILIZA JUU YA PAA - HABARI MPYA

..

ASHTAKIWA KWA KUENDESHA GARI KICHWA KIKIWA KIMEPITILIZA JUU YA PAA


Mwanaume mwenye urefu wa futi 6.7 ambaye mwanzo alikataa kuwa hakuwahi kusimama akiwa anaendesha gari dogo sasa amekiri kuwa ana hatia katika dakika za mwisho za kusikilizwa kesi inayomkabili na kukiri kuwa alishawahi kukutwa na makosa mengine 12 yanayohusiana na kukiuka sheria za usalama barabarani.


Adam Elliott, mwenye miaka 26, anayeishi jijini Newcastle nchini Uingereza, ameshitakiwa kwa kuhatarisha usalama baada ya kuendesha gari katika daraja la Tyne akiwa na gari lisilo na paa (convertible) aina ya Ford Ka huku kichwa chake kikiwa kinaonekana kutokeza juu kabisa ya gari hilo.


Jana alisisitiza kuwa alikuwa makini kabisa wakati akiendesha gari hilo na Nick Cartmell, akimtetea, aliiambia Mahakama ya Kifalme jijini Newcastle kuwa: ‘Ana uhakika kuwa hakuendesha gari hiyo akiwa amesimama.
Leo Adam amekiri mbele ya Mahakama hiyo kuwa kwa yeye kuendesha gari hiyo kunahatarisha usalama lakini gari yenyewe ni fupi kulinganisha na urefu wake, akiongezea kwa kusema: ‘Mimi ni dereva mzuri sana’.


Elliott, ambaye ni kiongozi wa kampuni ya “I Buy Any Car North East”, alisema alikuwa akiipeleka gari hiyo kwa mteja wake.

Akiongea baada ya kusikilizwa kwa kesi yake hiyo nje ya Mahakama ya Kifalme jijini Newcastle, Adam alisema: ‘Sikusimama, mimi ni mrefu tu.’


Adam Elliott, nje ya mahakama ambapo alisisitiza kuwa wakati anaendesha gari hilo hakuwa amesimama ingawa amekubali mahakamani kuwa ana makosa. The court heard he had 12 previous convictions of driving while disqualified.

‘Nilikubali kuwa na hatia katika kesi hii kwakuwa nilishauriwa kufanya hivyo na mwanasheria wangu, lakini bado nasisitiza kwamba sikuwa naendesha gari huku nimesimama. Tatizo ni kwamba mimi ni mrefu sana.


‘Mimi ni dereva mzuri sana ila nilishauriwa kukubali makosa ili kesi dhidi yangu iishe,’ alisema.

Akiiahirisha kesi hiyo ili itolewe maamuzi mwezi ujao, Jaji Robert Adams alisema: ‘Ni wazi kabisa kuwa ulikuwa unajionesha kwa makusudi kuonesha urefu wako kwa watu kwa kuendesha gari ya wazi ambayo ni fupi.

‘Ni wazi kabisa ulifanya kusudi ili madereva wengine wakuone. Kitendo hiki kilikuwa ni hatari kukifanya.’

Jana, kituo cha Chronicle Live kilimkariri wakili wa Adam, Nick Cartmell akisema wakati anamtetea mteja wake akiiambia Mahakama kuwa: ‘Anakubali kuwa kichwa chake kilikuwa juu ya gari aliyokuwa anaiendesha lakini hakuwa amesimama na alikuwa akiimiliki vizuri gari hilo, ni gari dogo sana.’

Related Posts

Post a Comment