const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); WENGER ATAVUNA FAIDA YA HASIRA ZAKE - HABARI MPYA

..

WENGER ATAVUNA FAIDA YA HASIRA ZAKE


Kocha wa washika bunduki wa London, Arsene Wenger aliamua kujichukulia sheria mkononi baada ya kukorofishana na mwamuzi wa akiba Anthony Taylor katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliopigwa katika dimba la Emirates Jumapili iliyopita dhidi ya klabu ya Bunley.

Mechi hiyo iliyoisha kwa Arsenal kushinda 2-1 ilionesha kumpa “stress” mzee Wenger na kuamua kukorofishana na Taylor baada ya Buley kupata penati dakika ya 93 na kumwita mwamuzi aliyekuwa akichezesha pamano hilo kuwa ni “muongo”. Penati hii ilifanya mpaka muda huo timu hizo ziwe zimefungana goli 1-1, lakini dakika nne baadae Arsenal ilipata goli la pili lililofungwa na Alexis Sanches kupitia penati. Wenger aliomba msamaha kupitiavyombo vya habari lakini FA imemtaka ajieleze ni kwa nini asipewe adhabu kutokana na nidhamu mbaya ya kimchezo aliyoinesha.

Kutokana na ukorofi huu, Wenger anakabiliwa na adhabu kali ya kukosa baadhi ya mechi ambazo inadhaniwa kuwa hazitapungua nne. Hii inasababisha kutokuwepo kwenye benchi la ufundi katika mechi ngumu ya timu yake dhidi ya Chelsea utakaochezwa February 4.

Akikosa mechi hii bila shaka itaweza kuathiri matoke ambayo timu hiyo itayapata kwakuwa katika mechi zenye uzito wa aina hii, uwepo wa kocha mkuu katika benchi husaidia kuiweka timu katika mchezo.

Related Posts

Post a Comment