const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Prof. Kitila Mkumbo aipongeza Hatifungani ya NMB kwa kukusanya bilioni 400 - HABARI MPYA

..

Prof. Kitila Mkumbo aipongeza Hatifungani ya NMB kwa kukusanya bilioni 400


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ameipongeza benki ya NMB kwa kuweka rekodi ya bilioni 400 za mauzo ya Hati Fungani ya NMB Jamii Bond ikiwa ni zaidi ya mara tatu ya lengo lililokusudiwa ambapo ni Tsh Bilioni 212.9 kwa fungu la shilingi za kitanzania na dola za kimarekani milioni 73 kwa fungu la dola.

Amezungumza hayo leo Disemba 12, 2023 wakati wa hafla ya kuiorodhesha Hati Fungani ya NMB Jamii katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ambapo fedha zote zilizopatikana kupitia Hati Fungani ya Jamii zitaelekezwa katika kutoa mikopo nafuu kwenye miradi endelevu ikiwemo miradi ya nishati mbadala, miradi ya kuzuia na kudhibiti uchafuzi wa mazingira, miradi ya maji, miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, miradi ya wanawake, vijana, elimu, afya, nyumba nafuu na mingine inayoendana na hiyo.


 “Hati Fungani ni fursa muhimu kwa jamii kunufaika kwa njia mbili za kuweka akiba lakini pia kufanya uwekezaji wenye faida kubwa, bond ni mkopo ambao Taasisi ya fedha inakopa kwa Wananchi, NMB ingeweza kwenda kukopa BoT au Benki za nje lakini ikachagua kukopa kwa Wananchi kupitia mdhamana wao ambaye ni CMSA na inarejesha kwa riba kubwa ya asilimia 9.5” ameongeza

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) CPA Nicodemus Mkama amesema kutokana na mazingira wezeshi yanayotolewa na Serikali yamekuwa na matokeo chanya katika maendeleo ya Sekta ya Fedha, hususan masoko ya mitaji ambapo thamani ya uwekezaji katika masoko ya mitaji imeongezeka kwa asilimia 7.6 na kufikia shilingi trilioni 36.13 katika kipindi kilichoishia Novemba 2023, ikilinganishwa na shilingi trilioni 33.59 katika kipindi kilichoishia Novemba 2022. 

Ameongeza kuwa thamani ya uwekezaji katika Hatifungani za Serikali na Hatifungani za Kampuni imeongezeka kwa asilimia 18.0 na kufikia Shilingi trilioni 19.76 katika kipindi kilichoishia Novemba 2023, ikilinganishwa na Shilingi trilioni 16.75 katika kipindi kilichoishia Novemba 2022.Mhe Mgeni Rasmi, Kwa mantiki hii, leo kutokana na korodheshwa kwa hatifungani ya NMB, thamani ya uwekezaji katika Hatifungani za Kampuni inaongezeka kutoka Shilingi bilioni 325.39 na kufikia Shilingi bilioni 721.13 sawa na ongezeko la asilimia 121.62.


Hivyo nitoe rai kwa wadau wote wa masoko ya mitaji kuendelea kushirikiana na Serikali kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana katika kutekeleza mikakati ya kuendeleza masoko ya mitaji hapa nchini ikiwemo kuleta bidhaa mpya katika masoko haya ambazo zitaweza kuorodheshwa katika Soko la Hisa ili pamoja na mambo mengine kuwapatia wawekezaji taarifa mbalimbali kuhusiana na bidhaa hizo ikiwemo bei kwa namna iliyo wazi. Kwa kufanya hivyo tutawezesha masoko ya mitaji kuendelea kuwa injini ya kuchochea maendeleo na ukuaji wa uchumi wa nchi yetu amesema CP Mkama

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Ruth Zaipuna amesema NMB Jamii Bond ilikuwa imegawanyika katika mafungu mawili, fungu la kwanza likihusisha shilingi za kitanzania na fungu la pili la dola za kimarekani ambako kote wamevuka lengo la makusanyo kwa kupata shilingi bilioni 212.9 kutoka bilioni 100 za lengo na upande wa dola wakikusanya milioni 73 badala ya milioni 15 walizolenga.

“Kwa mantiki hiyo, thamani ya jumla ya fedha zilizopatikana kutokana na NMB Jamii Bond ni Sh. Bilioni 400, ambazo ni mara tatu zaidi ya lengo tulilokuwa nalo” amebainisha Ruth Zaipuna huku akiwahakikishia Wateja zaidi ya 5,600 walionunua Hati Fungani hizo kuwa pesa zao ziko mikono salama.

 


Related Posts

Post a Comment