Kuna stori nikizipata uwa lazima nihakikishe nakusogezea sasa hii ni ya Jamaa mmoja atatumikia kifungo cha muda jela baada ya kumuadhibu mkewe kwa njia ya kushangaza. Moses Okello aliwashangaza watu kwa kutia pilipili kali kwenye nguo za ndani za mkewe kisha kumshawishi azivae nchini Uganda.
Okello,ambaye ni mkazi wa kijiji cha Barmola alifikishwa mahakamani February 1, 2018kueleza sababu kwa nini alitia pilipili kwenye nguo za ndani za mpenzi wake. Ni baada ya mkewe kulalamika kuwa sehemu zake za siri zilikuwa zimeanza kuvimba na kuwasha alienda kwa Daktari na ikabainika kuwa Mumewe aliweka pilipili kwenye nguo zake za ndani.
Mwanamke huyo aliiambia Mahakama “Nilianza kuwashwa baada ya kuvaa nguo hizo. Hata nikioga, mwasho hukuisha,”.
Alipopewa nafasi ya kujitetea Okello aliiomba Mahakama msamaha akisema hakujua kama ingeweza kuleta madhara kwani yeye alichukulia kama utani kwa mke wake. Mahakama imemhukumu kutumikia kifungo cha siku 40 jela…
Post a Comment
Post a Comment