Uamuzi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam kuongeza siku za uuzwaji wa hisa za awali za kampuni ya simu ya Vodacom nchini umeibua wasiwasi miongoni mwa wawekezaji ambao hawafahamu hatma ya fedha walizowekeza.
Wataalamu wameeleza wasiwasi wao kwamba hali hiyo inaweza kuwavunja moyo wawekezaji wachanga ambao wanakadiriwa kufikia 40, 000 ambao walinunua hisa za awali za vodacom kwa ajili ya kuwekeza kwenye manunuzi ya hisa zijazo.
Wengine walikuwa na mashaka kwamba hali hiyo inaweza kutia doa kwa makampuni mengine ya simu nchini ambayo yanatarajiwa kuanza kuuza hisa zao za awali siku za hivi karibuni baada ya mamlaka ya dhamana na mitaji, Jumamosi iliyopita kuagiza kusogezwa mbele tarehe ya manunuzi ya hisa hizo.
Maamuzi ya kusogezwa mbele uuzwaji wa hisa za awali za makampuni ya simu nchini yanawapa fursa pia wawekezaji wakigeni kuweza kushiriki kwenye manunuzi ya hisa za awali.
Sheria ya Fedha ya mwaka 2016 imeifanyia marekebisho sheria ya mawasiliano ya kielekroniki na posta ya mwaka 2010, ambayo inayataka makampuni yote ya simu nchini kuuza sio chini ya asimilia 25 ya hisa zao kwenye soko la hisa la Dar es salaam ili kuboresha umiliki wa ndani.
Hata hivyo, sheria ya fedha ya mwaka 2017, mnamo mwezi wa saba, pamoja na marekebisho mengine, iliifanyia marekebisho sehemu ya 26 ya sheria ya mawasiliano ya kielekroniki na posta ya mwaka 2010 ili kuruhusu wawekezaji wa kigeni kushiriki kwenye manunuzi ya hisa za awali.
Marekebisho hayo pia yametoa ruhusa kwa makampuni ya simu nchini kuorodhesha chini ya asilimia 25 ya hisa zao baada ya mamlaka ya dhamana na mitaji kumshauri Waziri wa fedha na mipango namna ya kufanya endapo kampuni itashindwa kupata kiasi cha fedha kilichopangwa kwenye hisa za awali.
“Kumekuwa na hali ya kutoelewa miongoni mwa wawekezaji wachanga wa wazawa ambao waliwekeza kwenye hisa za awali na wamekuwa wanasubiri kwa zaidi ya wiki saba tangu kufungwa kwa zoezi hilo. Wamekuwa wanajazana kwenye ofisi za mamlaka ya dhamana na mitaji kupata ufumbuzi wa kinachoendelea, lakini hakuna majibu sahihi yalitotolewa. Hii inaweza kusababisha hali ya kutoaminiana na kuathiri makampuni mengine ya simu nchini ambayo yatauza hisa zao za awali siku za hivi karibuni,” alisema muuzaji ambae hakutaka jina lake litajwe.
Haya yote yametokea baada ya watanzania ambao walinunua hisa zao miezi mitatu iliyopita wamekuwa wanasubiri vyeti vyao vya hisa na wamekuwa wakisubiri mamlaka ya dhamana na mitaji waruhusu na kutaja tarehe ya utolewaji wa vyeti hivyo vya hisa.
Zainabu Juma,umri miaka 26, ambae ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam alisema kwamba alinunua hisa zenye thamani ya shilling 170, 000 miezi mitatu iliyopita, lakini hafahamu nini kitatokea.
Wasiwasi wake mkubwa ni kwamba atapoteza fedha yake. Alisema kwamba alidunduliza kwa miaka miwili kupata hiyo fedha na aliamua kuwekeza kwenye hisa za vodacom, alisema alishawishika kuwekeza baada ya kumuona Waziri mkuu alikinunua hisa za vodacom hadharani.
“nimeenda kwenye ofisi za mamlaka ya dhamana na mitaji mara mbili lakini wamekuwa wananambia nisubiri pasipo kutoa taarifa kamili kuhusiana na lini hasa nitapata cheti cha hisa zangu, ” alisema.
Post a Comment
Post a Comment